Stori yangu

Nilitaka kuwasaidia watu wengine waandike vitabu lakini sikujua nianze wapi kuwafikia watu wote.

Nilipotoa kitabu changu cha kwanza mwaka 2017 mwishoni sikuwa nafahamu mambo mengi na sikuwa na mtu wa kunisaidia. Kitabu kilitoka lakini hakikuwa natika ubora niliotegemea na sikujua nifaye nini kuboresha makosa. Ndiposa niliamua kutafuta kozi mbalimbali za uandishi wa vitabu mtandaoni na kuanza kuuliza kwa waandishi walionitangulia.

Nilijua mambo mengi mno na sasa kiu yangu ikawa kukusaidia wewe upate kitabu bora na ujue hasa mchakato wa kutoa kitabu ukoje. Wakati nawaza naanzaje kukusaidia ndipo likaja wazo la kuanzisha blogi ambayo nitaweka mafunzo na makala mbalimbali.

Blogi hii ya DaudiPages ni mahsusi kwa ajili yako. Kila siku lipo jambo utajifunza hapa. 

Ni mimi Daudi Lubeleje, Mwandishi wa vitabu

Ninayejali mafanikio yako

UNATAKA NIANZE KUKUSAIDIA JAMBO LIPI KATI YA HAYA?

Nataka nianze kuandika kitabu...

Nitakufundisha mbinu rahisi sana za kuandika kitabu chako.

Nitakupa mazoezi ya kuandika na kukufatilia hatua kwa hatua

Nataka nitoe kitabu changu ila sijui nianzie wapi...

Nitakufundisha hatua unazotatakiwa upitie ili kutoa kitabu chako bila stress

Utapata huduma bora ya ubunifu wa jalada la kitabu, sanifu kurasa na n.k

Nataka nijue mbinu za kuuza kitabu changu zaidi...

Nitakufundisha jinsi ya kujenga mfumo rahisi wa kuuza kitabu popote bila kutumia nguvu nyingi

Nitakupa mwongozo wa kupata wa kutengeneza jukwaa lako kama muandishi

Nialike kuzungumza

Una semina, warsha, kongamano, au tukio lolote muhimu?

Weka booking tuongee zaidi


.