[Kozi] Hatua nne katika uandishi wa vitabu


[Kozi] Hatua nne katika uandishi wa vitabu

Unazifahamu hatua nne (4) katika uandishi wa vitabu?. Watu wengi hufikia hatua ya kwanza, wengine hatua ya pili na ya tatu, na wachache sana huifikia hatua ya nne. Kuhusu hatua hizi nne (4), fahamu kwamba hatua zote nne zina uzito sawa, halafu zinategemeana, na zinaenda kwa mtiririko kwa kupandiana. Mwandishi hawezi kwenda hatua ya pili, bila ya kupitia hatua ya kwanza.

Je! Hatua hizo nne ni zipi? Tuanze kumla tembo wetu sasa.

Hatua ya kwanza ni KUANDIKA.

Ukitaka kuwa mwandishi wa vitabu sharti uandike kwanza. Iwe wewe mwenyewe utaandika, au utaandikiwa na mwingine, lakini lazima stori yako au maudhui yako yaandikwe.

Hii ndiyo hatua ya kwanza. Karatasi tupu haiwezi kuwa kitabu!. Safari ya kuwa mwandishi inaanza na kuandika. Kaa chini na andika story yako unayotaka iende kwa wasomaji. Kaa chini na andika yale maudhui unataka yafike kwa wasomaji.

Watu wengi hufanikiwa katika hatua hii. Lakini kwa bahati mbaya, vile vitu vingi ambavyo watu wanaandika (bila shaka hata wewe umeandika tayari) wanashindwa kutembea navyo kwenda hatua ya pili katika uandishi ili kukamilisha ndoto zao. Kuishia katika hatua hii ya kwanza hakukufanyi kuwa mwandishi. Kama umeshaandika tayari, fanya juhudi usibakie katika hatua hii ya kwanza ya kuandika tu, bali nenda hatua ya pili.

Kama bado hujaandika, unaanzaje? Nafikiri hili linaweza kuwa swali la wengi. Naanzaje kuandika?
Unaanza kuandika kwa kuamua kuandika!. Anza kuandika story yako Facebook, Twitter, WhatsApp au Instagram. Kama unaweza kupiga story kwa masaa matatu na kuzungumza maneno yote hayo huwezi kushindwa kuhamisha hayo maneno kwenye karatasi.

Fanya blogging. Andika machapisho yako na yaweke mtandaoni kwenye blogu. Safari ya uandishi ndivyo inavyoanza hivyo. Hakuna muujiza mwingine wa kuwa mwandishi isipokuwa kuandika kwanza. Kumbuka tu, hii ni hatua ya kwanza itakayokupeleka hatua ya pili. Je! Hatua ya pili ni ipi?

Ili kuendelea kusoma hatua tatu zilizobakia, soma kozi hii katika majukwaa yafuatayo, chagua jukwaa unalopenda

Kwa maswali na maoni, tuandikie hapa chini

.