Badilisha maisha yako kwa kusoma kozi hizi nane (8)


Badilisha maisha yako kwa kusoma kozi hizi nane (8)

Katika maswali haya, ni swali lipi linakuelezea wewe na umekuwa ukijiuliza bila majibu yake, na sasa ungetaka kuchukua hatua ya kufanyia kazi?; Je mimi nataka kujua jinsi ya kuandika kitabu? Je mimi nataka kujua jinsi ya kuuza kitabu changu zaidi? Je mimi nataka kutoa kitabu changu ila sijui nianzie wapi? Au Je mimi nataka kuwa bora zaidi kwenye uandishi wa vitabu?. Majibu yamepatikana, nakupa njia rahisi ya kutusua.

Ni hivi, nimekukusanyia kozi nane (8) tofauti tofauti za uandishi wa vitabu. Unachotakiwa kufanya wewe ni kuchagua ile kozi unataka na kuanza kuisoma mara moja. Usichelewe, anza leo.

Kozi ya 1 | Hizi ndizo sababu kitabu chako hakiuzi

Umeandika kitabu, umetumia gharama kukiandaa na kukitoa halafu ili
iweje? Si uuze uingize pesa siyo?. Bila kumung’unya maneno, kila
mwandishi anataka auze nakala za kutosha aingize pesa.

Ada: Tsh. 2000 tu! > Anza kusoma

Kozi ya 2 | Kama mwandishi wa vitabu, unataka kufanikiwa kwenye nini?

Wewe kama mwandishi unataka kufanikiwa kwenye nini?

  1. Kupiga pesa
  2. Kufikia wasomaji wengi zaidi na ujue vitabu vyako vinapendwa
  3. Kupata michongo ya biashara
  4. Kujulikana tu kama nawe ni mwandishi au mtaalamu kwenye eneo unaloandika
  5. Kushinda tuzo za uandishi

Ada: Tsh. 2000 tu! > Anza kusoma

Kozi ya 3 | Njia tatu (3) zilizo thibishwa za kuandika kitabu

Usipate stress unapotaka kuandika kitabu. Kwenye kozi hii
nimekushirikisha njia tatu ambazo zimethibitishwa kabisa za kuandika kitabu. Unachofanya wewe ni kuchagua njia itakayokufaa.

Ada: Tsh. 2000 tu! > Anza kusoma

Kozi ya 4 | Saikolojia ya msomaji anaponunua kitabu

Kuuza kitabu ni ujuzi ambao kila mwandishi anapaswa awe nao. Mafanikio ya mwandishi kwa kiasi kikubwa tunayapima kwa kuangalia mwandishi ameuza
nakala ngapi.

Ada: Tsh. 2000 tu! > Anza kusoma

Kozi ya 5 | Hatua nne (4) katika uandishi wa vitabu

Unazifahamu hatua nne (4) katika uandishi wa vitabu?
Watu wengi hufikia hatua ya kwanza, wengine hatua ya pili na ya tatu, na wachache sana huifikia hatua ya nne.

Ada: Tsh. 2000 tu! > Anza kusoma

Kozi ya 6 | Ujuzi wa kuhariri kitabu

Kitabu chenye makosa kinamwondolea ladha nzuri na tamu msomaji. Kwa hiyo kukipitia na kukihariri kitabu chako ni jambo lisilokwepeka. Lakini, si waandishi wengi hufanya hivyo.

Ada: Tsh. 2000 tu! > Anza kusoma

Kozi ya 7 | Mambo ya kuandaa kupata jalada bora la kitabu

Nilianza kudizaini makava ya kitabu mwaka 2018 nilipoanza kufanya kazi na DL Bookstore. Kadiri siku zinaenda nayaona mabadiliko kwenye tasnia ya uandishi wa vitabu Tanzania, kwani nashuhudia jinsi

Ada: Tsh. 2000 tu! > Anza kusoma

Kozi ya 8 | Jinsi ya kuandika na kutoa eBook

Katika kozi hii utajifunza, kutaja kwa uchache mambo yafuatayo; Jinsi ya kupata mawazo ya kuandika ebook, Hatua 6 za kuandika ebook, Unapataje muda wa kuandika ebook, na n.k

Ada: Tsh. 5000 tu! > Anza kusoma

Kozi bado hazijaisha ila hapa nimekukusanyia chache tu. Unataka kuona nyingi zaidi? Nenda hapa kuona kozi nyingi zaidi

.